MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA
MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujajiingiza kwenye biashara. Nimekuwekea baadhi ya mambo hayo hapa chini. Haya ni yale niliyojifunza on the ground ndani ya miaka yangu michache hii ya ujasiriamali toka mwaka 2021 katika biashara mbali mbali nilizofanya. Ukiyazingatia utaona faida yake. 1. HAKIKISHA UNA ELIMU YA BIASHARA Simaanishi diploma sijui certificate ya chuo au zile notes za Commerce. No. Hiyo siyo elimu ninayomaanisha. Namaanisha aina ya elimu kwa vitendo kama vile apprenticeship. Yaani kujifunza kwa mtu taratibu uone jinsi biashara inavyofanyika. Kama hilo ni gumu kulingana na mazingira basi hakikisha biashara unayotaka kuifanya au mradi unaotaka kuanzisha una watu wanaofanya kitu hicho hicho walio tayari kukupa elimu kila siku hasa miaka miwili ya kwanza katika jambo hilo. Watu watakaokuwa tayari kukupa siri za mafanikio bila kukuficha. Watu watakaokuwa tayari kukushika mkono kwa dhati mpak...