MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujajiingiza kwenye biashara. Nimekuwekea baadhi ya mambo hayo hapa chini. Haya ni yale niliyojifunza on the ground ndani ya miaka yangu michache hii ya ujasiriamali toka mwaka 2021 katika biashara mbali mbali nilizofanya. Ukiyazingatia utaona faida yake. 1. HAKIKISHA UNA ELIMU YA BIASHARA Simaanishi diploma sijui certificate ya chuo au zile notes za Commerce. No. Hiyo siyo elimu ninayomaanisha. Namaanisha aina ya elimu kwa vitendo kama vile apprenticeship. Yaani kujifunza kwa mtu taratibu uone jinsi biashara inavyofanyika. Kama hilo ni gumu kulingana na mazingira basi hakikisha biashara unayotaka kuifanya au mradi unaotaka kuanzisha una watu wanaofanya kitu hicho hicho walio tayari kukupa elimu kila siku hasa miaka miwili ya kwanza katika jambo hilo. Watu watakaokuwa tayari kukupa siri za mafanikio bila kukuficha. Watu watakaokuwa tayari kukushika mkono kwa dhati mpak...
*SELL YOURSELF FIRST BEFORE THE PRODUCT* Makala hii imeandaliwa na Emmanuel Mwambene~ Mwandishi wa Vitabu & Mfanyabiashara. Kauli “Sell yourself first before the product” ina uzito mkubwa sana katika biashara. Ina maana kwamba kabla mteja hajavutiwa na bidhaa au huduma yako, lazima kwanza akuamini wewe kama mtu. Hii ni kanuni ya msingi katika uuzaji (sales) na ujasiriamali kwa ujumla. Hapa ni jinsi inavyofanya kazi kibiashara: --- 1. Uaminifu ni msingi wa biashara Wateja hawanunui tu bidhaa – wananunua imani kwa muuzaji. Kama huonekani mwaminifu, mkweli, au mwenye kujali, hata bidhaa nzuri inaweza kukataliwa. --- 2. Mahusiano kabla ya biashara Watu hununua kwa watu wanaowapenda, wanaowaamini, au walio na mahusiano nao. Ukijijenga vizuri – kwa mawasiliano mazuri, kuaminika, na huruma – bidhaa zako zitafuata tu. --- 3. Wewe ni chapa ya biashara yako Haswa kwa biashara ndogo ndogo au biashara za mtu binafsi, wewe mwenyewe ni nembo ya kwanza. Tabia zako, mawasiliano, ...
Comments
Post a Comment